Ndoto Hub ni jukwaa mahususi la kuwawezesha wanawake wajisiriamali wabunifu kuanzisha biashara zenye kumuendeleza yeye na jamii yake. Kupitia Ndoto Hub, utapata eneo la kufanyia kazi ndoto yako, mafunzo na nyenzo za ukuzaji na uongozaji biashara na stadi za maisha kumudu na kujitambua.

Soma Vigezo na Masharti:

Kwa kujiunga na Ndoto hub, muombaji anakubaliana na vigezo na masharti yafuatayo:

  • 1. Muombaji ni msichana/mwanamke mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18) na usiozidi miaka thelathini na tano (35)

  • 2. Muombaji ndio Muasisi au muasisi-mwenza wa wazo analoombea

  • 3. Ushiriki wa Ndoto Hub ni wa hiari, muombaji yuko tayari kufuata muongozo na utaratibu unaotolewa na uongozi wa Ndoto Hub, Shule Direct na wadau wake

  • 4. Ndoto Hub, Shule Direct na wadau wake wana uamuzi wa mwisho juu ya nafasi za Ndoto Hub

  • 5. Muombaji anathibitisha kuwa taarifa zote alizotoa ni kweli na sahihi

  • 6. Nafasi anayopewa muombaji kujiunga na Ndoto hub haihamishiki

  • 7. Muombaji yuko tayari kutoa ushirikiano na taarifa zake za kibiashara au nakala, picha mnato au ‘video’ kwa uongozi wa Ndoto Hub, Shule Direct na wadau wake kwa malengo ya utafiti au kutoa taarifa kwa wadau

  • 8. Muombaji anathibitisha utayari wake wa kushiriki mafunzo kwa muda wa wiki kumi (10) kwenye eneo la Ndoto Hub lililoko #539 Msasani, Old Bagamoyo Road, Dar es Salaam na kuwa muombaji atajigharamia kuwepo eneo la mafunzo kwa kipindi chote cha wiki 10

  • 9. Wasilisha maombi kabla ya tarehe 19/05/2019 saa moja kamili jioni.

Tutumie ndoto yako sasa kujiunga.

Bofya hapa Kujiunga

Wasilisha maombi kabla ya tarehe 19/05/2019 saa moja kamili jioni.